Burudani ya Michezo Live

Mwalimu wa dance aliyewahi kucheza na Usher, Emanuel Austin kuja Dar kutoa mafunzo na msaada

Mwalimu wa dance, Mtanzania aishiye nchini Ujerumani, Emanuel Austin, anatarajia kuja jijini Dar es Salaam, Oct 15 kwa shughuli za msaada na kufundisha watoto kucheza muziki.

IMG-20131007-WA000

Mwalimu huyo ataambatana na mchumba wake wake ambapo amepanga kutembelea baadhi ya shule pamoja na mambo mengine na watakaa kwa siku 10.

IMG-20131007-WA001

Emanuel alizaliwa tarehe 27.10.1990 jijini Dar es Saalam lakini amekuwa akiishi nchini Ujerumani na wazazi wake kuanzia mwaka 1996. Akiwa na umri mdogo alikuwa akipenda kuigiliza namna wanavyocheza wasanii, Michael Jackson na kujikuta akipenda zaidi kucheza hip-hop.

993356_528154187233374_1361970201_n

Mwaka 2006 alishinda shindano la vipaji vya kucheza huko Hanau, Ujerumani. Mwaka 2008, alianza kufundisha masomo ya kucheza na kujikita zaidi katika hip hop, michezo ya watoto na Salsa Cubana. Pia amekuwa akifundisha kucheza Merengue na Bachata.

IMG-20131007-WA002

Mpaka sasa, Emanuel Austin anafanya kazi kwenye shule kubwa ya dance nchini Ujerumani na ameshacheza kwaajili ya mastaa Don Omar, Jason Derulo na Usher huku pia akifanya kazi kama model.

IMG-20131007-WA003

Msikilize zaidi hapa akihojiwa kwenye kipindi cha Urban Top 10, cha CG FM, Tabora.

Mfahamu zaidi kwa kutembelea ukurasa wake wa Facebook hapa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW