Michezo

Mwamuzi aliyempatia kadi nyekundu mchezaji afungiwa

Kamati ya nidhamu ya Ligi ya Kuu nchini Ufaransa hapo jana siku ya Alhamisi imetoa adhabu ya kifungo cha miezi sita kwa mwamuzi, Tony Chapron kufuatia kumpiga teke na kumpatia kadi nyekundu beki, Diego Carlos wakati wa mchezo dhidi ya Paris Saint-Germain.

Chapron alimpiga teke beki huyo kufuatia kitendo chake cha kumgonga mwamuzi huyo na kupelekea kuanguka chini hali aliyotafsri ni makusudi na kuamua kumrudishia kwa kumpiga mguuni na kumzawadia kadi ya pili ya njano.

Hapo hawali kamati ya nidhamu ya ligi ya Ufaramsa ilimfungia mwamuzi huyo kwa muda usiyojulikana kabla ya kuja na maamuzi hayo ya kifungo cha miezi sita.

Kadi aliyotoa mwamuzi huyo kumpatia Diego Carlos imebatilishwa katika mchezo huo PSG ilichomoza na ushindi wa bao 1-0.

Chapron amekuwa mwamuzi katika ligi kuu ya Ufaransa tangu 2004 na amesimamia zaidi ya mechi 400, ikiwa ni pamoja na fainali ya Kombe la Ufaransa mwaka 2014.

Kabla ya tukio hilo mwamuzi huyo alitangaza kutundika daluga mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi ya Hispania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents