Michezo

Mwamuzi wa pambano la Joshua vs Parker mwezi huu atangazwa rasmi

Mwamuzi wa pambano la masumbwi la uzito wa juu, Anthony Joshua dhidi ya Joseph Parker, Giuseppe Quartarone ametangazwa rasmi kusimamia pambano hilo kubwa duniani.

Bondia, Anthony Joshua (kulia) na Joseph Parker (kushoto)

Quartarone raia wa Italia atakuwa mwamuzi wa mchezo huo ambao Joshua atautetea ubingwa wake wa WBA na IBF dhidi ya bingwa wa WBO, Parker katika uwanja wa Cardiff machi 31.

Mwamuzi, Giuseppe Quartarone

Mwamuzi huyu alishawahi kusimamia mapambano mbalimbali ya uzito wa juu likiwemo la Alexander Povetkin’s ubingwa wa WBA dhidi ya Cedric Boswell mwaka 2011 pia alishawahi kusimamia mabondia kama, Brits Scott Quigg, Martin Murray na Enzo Maccarinelli.

Parker raia wa New Zealandoi amewasili Uingereza wikiendi hii akiwa na mwalimu wake Kevin Barry tayari kwa mchezo huo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents