Mwana FA aiomba serikali iurudishe mfumo wa analojia

Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa mfumo wa digitali unawaumiza.

faaa

Akiongea na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye ving’amuzi.

“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.

Alisisitiza kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents