Burudani

Mwana FA alitaka ‘tuwasurprise’ watu – Country Boy

Rapper kutoka kwenye Bongo Flava, Country Boy amesema sababu ya kuweka usiri wa kolabo yake na Mwana FA ni kutoka kuwashangaza watu kwa muziki mzuri.

Country Boy ambaye Juzi July 9 aliachia ngoma mpya ‘Turn Up’ akiwa amemshirikisha Mwana FA, ameiambia Ladha 3600 ya E Fm kuwa walifanya hivyo kuepuka watu kujua ngoma ya aina gani inakuja.

“Unajua idea yote imetokana na Mwana FA alitaka tuwa-surprise watu, mtu akipata picha ninafanya ngoma na Mwana FA wakati huo huo amefanya na Bill Nass mtapata picha ni ngoma fulani ya rap, kwa hiyo atajua ni kitu gani kimefanyika na itakuwa haina nguvu ndio maana tumetaka tuwashtukize kwa sababu tunaamini ni ngoma kali,” amesema Country Boy.  

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents