Burudani

Mwana FA: Sijawahi kukaa na baba yangu maisha yangu yote (Video)

Pengine hukuwa unalijua hili. Mwana FA hajawahi kuishi na baba yake katika maisha yake yote.

FA ametuambia hilo baada ya kumuuliza tofauti ya malezi aliyoyapata kutoka kwa baba yake na yale anayompa mwanae wa kike, Malikah.

“Mimi sijawahi kukaa na baba yangu maisha yangu yote,” anasema.

“Nimekuwa naruka ruka sana, mara nakaa kwa shangazi yangu, mara nakaa kwa babu yangu, kwa bibi yangu ndiyo kwetu ilikuwa, kwa shangazi yangu mwingine hivyo,” ameongeza.

“Experience niliyokuwa naiona ni kwa binamu zangu wanavyokaa na baba zao na mimi ninavyokaa na baba zao. Mimi cousins zangu fulani baba yao alikuwa akija hawakai tena sebuleni. Yaani muda wenu wa kuangalia TV unakishwa mzee akiingia nyumbani. Either hilo au TV itatolewa usiku mzee akatika kwenda kulala itarudishwa ndani.”

Mwana FA amesema malezi anayompa mwanae ni tofauti kidogo.

“Mimi mtoto wangu ananiona kama mshkaji wake naona,” anasema.

“Mimi na yeye ni marafiki. Atakaa ataangalia katuni zake na siwezi hata kuangalia mpira, atataka kunieleza wale katuni wake kila mmoja anaitwa nani.”

FA anaamini kuwa wazazi wengi wa sasa wamegundua kuwa ni vizuri zaidi wakawa karibu na watoto wao kuliko wakiwaogopa.

12298829_1058336640872644_662653160_n

“Namna ambayo maisha mimi nimekua, sitaki mwanangu apitie hata robo yake,” anasisitiza. “Kazi nitakayoifanya ni kumpa mafunzo niliyoyapata kutokana na hustle niliyokuwa naipitia bila yeye kuipitia hiyo hustle.”

Malikah ana umri wa miaka minne sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents