Aisee DSTV!

Mwanadada anayedaiwa kuvunja mahusiano ya Offset na Cardi B aomba msamaha

Mahusiano ya Cardi B na Offset yalidumu kwa muda mpaka kufanikiwa kupata mtoto, ni kitu ambacho kiliwaaminisha wengi kuwa wawili hawa watadumu kwa muda kwenye mahusiano yao.

Lakini majuzi mwanadada Cardi B aliweza kuweka wazi kuwa mahusiano yao yamevunjika rasmi na kauli hiyo ya Cardi B imemfanya mwanadada anayedaiwa kuwa ndio mchepuko wa Offset kufunguka na kuomba msamaha.

Mwanadada huyo anayejulikana kwa jina la Summer Bunni kupitia ukurasa wake wa Instagrama amefunguka na kusema ” Nasikia aibu, hii naieleza mimi kwenda kwa Cardi B, Mashabiki zake,Familia yake, na hali yake, hii haikuwa kusudio langu na sijawahi kuwaza kuvunja mahusiano na kuondoa furaha ya mtu na kumfanya mtu apewe talaka”

Hiyo ndio kauli ya Summer Bunni kwa ufupi kwenda kwa Cardi B ingawa bado haijawekwa wazi sababu hasa iliyopelekea mahusiano hayo kuvunjika.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW