Burudani ya Michezo Live

MwanaFA amuomba Mourinho aifunge Man United ”Tusaidie kumng’oa Babyface ili Poch apewe timu”

Usiku wa leo ligi kuu ya England kuna mechi kadhaa zinatarajiwa kuchezwa, lakini macho na maskio ya wapenzi wengi wa soka yataelekezwa pale Old Traffod, mahala ambapo kwa mara ya kwanza kocha mwenye maneno mengi zaidi Mreno Jose Mourinho atarejea, safari hii akiwa na kikosi kingine kabisa chenye uchu na shauku ya ushindi Tottenham akiwakabili waajiri wake wa zamani Manchester United.

Spurs ambayo inarekodi ya ushindi katika michezo yake mitatu iliyopita bila kupoteza chini ya Mourinho itawakabili United ambao wanaonekana kusuasua tangu kuanza kwa msimu huku lawama nyingi zikitupiwa kwa Ole Gunnar Solskjaer na wengine kudiriki hata kusema afukuzwe pengine mambo yatakuwa mazuri.

Shabiki kindakindaki wa Manchester United na msanii wa muziki nchini, MwanaFA amemuomba Mreno Jose Mourinho ambaye timu yake ya Tottenham itawakabili United kuwasaidia kumng’oa ‘Babyfac’ akimaanisha Ole Gunnar Solskjaer ili miamba hiyo inayopatikana katika viunga vya Old Traffod impatie kazi Mauricio Pochettino.

”Leo ndio ile siku mwanangu mwenyewe Mreno sio?kwa hiyo tunafanyaje?utusaidie kumng’oa Babyface ili Poch apewe timu yake ama utupe points tujikongoje,chaguo lako.” ameandika MwanaFA

Hapo jana kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, Mourinho amesema yeye na Manchester United wameshafunga ukurasa na kusisitiza ushindi kwenye mchezo wake wa leo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW