Moto Hauzimwi

MwanaFA kuipamba Miss Kanda ya..

Mwana FAMSHINDI wa tuzo ya albamu bora ya mwaka ya muziki wa Hip hop, Hamisi Mwinjuma ‘Mwanafalsafa’ ni miongoni mwa wasanii watatu watakaotoa burudani katika shindano la Miss Kanda ya Mashariki..

Mwana FANa Khadija Kalili

MSHINDI wa tuzo ya albamu bora ya mwaka ya muziki wa Hip hop, Hamisi Mwinjuma ‘Mwanafalsafa’ ni miongoni mwa wasanii watatu watakaotoa burudani katika shindano la Miss Kanda ya Mashariki litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Container, Kibaha mkoani Pwani.

Mbali ya Mwanafalsafa ambaye alishinda tuzo hiyo kwa albamu ya ‘Unanitega’, pia kutakuwa na wasanii wengine kama Vitalis Maembe anayetamba na kibao cha ‘Sumu ya Teja’ na Salum Wanne, maarufu kama Wanne Star.

Katika shindano hilo la funga kanda kwa Tanzania, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dk. Christine Ishengoma, ambako warembo 12 watashiriki kutoka mikoa ya Pwani, Lindi na Morogoro. Washindi watatu wa juu wataingia katika shindano la urembo la taifa.

Shindano hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Millennium Promotions chini ya ukurugenzi wake, Fortunatus Muganzi, limedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom, Redds’ Premium Cold (TBL), Daily News, Muzamil Katunzi, City Part Hotel – Sinza, Jenniffer Salon & Boutique – Kinondoni, Screen Masters, Mrs Mlawa Decoration – Kibaha na Max line International.

Warembo watakaochuana ni Sarah Kangezi, Sarome Kessy, Asha Ismail, Sarafina Mgumba, Restuta Pastory, Mwanesy Nyange, Hilda Hanzi, Queen Daud, Aysha Said na Amianata Omary.

Source: TanzaniaDaima

{mos_sb_discuss:6}

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW