Habari

Mwanafunzi auwa wenzake 17 kwa kuwapiga risasi

Mwanafunzi mwenye miaka 19 nchini Marekani, Nikolaus Cruz amewaua wenzake 17 kwa kuwapiga risasi, shambulio hilo lilitokea Florida.

Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa amebeba bunduki alianza kushambulia bila ya mpangilio nje ya shule hiyo kabla ya kushambulia ndani.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo, amesema mshambuliaji huyo alifukuzwa shule kutokana na utovu wa nidhamu. Tayari polisi wamemkamata kijana huyo.

Shirika la Upelelezila Marekani FBI limesema linashirikiana na polisi, kufanyia uchunguzi tukio hilo.

Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake wa twitter amewaondolea hofu raia wa Marekani, kwa kusema kuwa usalama upo kwa mtoto, mwalimu na mtu yeyote yule.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents