Habari

Mwanaharakati wa miaka 19 ashtakiwa kwa kutaka Hong Kong kujitenga na China

Mwanaharakati wa kutetea demokrasia huko Hong Kong mwenye umri wa miaka 19, ameshtakiwa kwa kosa la kuendeleza harakati za kuutenga mji huo kutoka China Bara.

Tony Chung ni mtu wa kwanza kushtakiwa chini ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyowekwa na China mjini humo.

Amefikishwa mahakamani siku mbili baada ya kukamatwa na polisi akishtakiwa pia kwa makosa ya utapeli wa pesa na kula njama ya kuchapisha habari za uchochezi.

Baada ya hapo alirudishwa rumande hadi Januari 7 wakati kesi yake itakaposikilizwa tena. Endapo atapatikana na hatia chini ya sheria hiyo mpya, basi atakabiliwa na adhabu ya kifungo cha takriban miaka 10 gerezani.

Chung ni mwanachama wa zamani wa kundi dogo la wanafunzi lenye imani kwamba huduma zinapaswa kudhibitiwa na kutolewa ndani ya Hong Kong kwa faida ya watu wake, imani inayochochea harakati za kutafuta uhuru wa eneo hilo kutoka China.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents