Habari

Mwanaharakati wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Ahmed Kathrad afariki dunia

Kiongozi na mwanaharakati aliyeshiriki kwa kiasi kikubwa katika kupambana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Ahmed Kathrad amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

Kathrad amefariki usiku wa kuamkia Jumanne hii katika hospitali ya mjini Johannesburg baada ya kuugua kwa kipindi kifupi kufuatia upasuaji aliofanyiwa katika ubongo wake.

Mwanaharakati huyo alikuwa ni mmoja ya watu nane kutoka chama cha African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 1964 akiwemo na Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi.

Kathrada alikaa jela kwa miaka 26 na miaka 18 kati ya hiyo alifungwa katika gereza hatari la Robben Island lililopo kwenye mji wa Cape Town. Aliachiliwa huru mwaka 1989.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents