Habari

Mwanajeshi mahakamani kwa wizi wa milioni 400/-

WAKAZI watatu wa Dar es Salaam akiwamo mwanajeshi, wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa tuhuma za wizi wa dola za Marekani 340,000 (zaidi ya Sh milioni 400) na vitu mbalimbali kwa kutumia silaha, mali ya Stephanen Ngoni.

Regina Kumba


WAKAZI watatu wa Dar es Salaam akiwamo mwanajeshi, wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa tuhuma za wizi wa dola za Marekani 340,000 (zaidi ya Sh milioni 400) na vitu mbalimbali kwa kutumia silaha, mali ya Stephanen Ngoni.


Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Dennis Mujumba aliwataja watuhumiwa kuwa ni Ofisa wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Otaiga (35) mkazi wa Mtoni Madafu wilayani Temeke.


Wengine ni Joseph Mwita (28) na Chacha Magiga (30), ambao wanadaiwa kutenda kosa hilo Juni 14, mwaka huu kwa kutumia bastola kabla ya kuiba katika eneo la Kinyerezi, Dar es Salaam. Mujumba alidai mbele ya Hakimu Mkazi Tonny Mbilinyi kuwa watuhumiwa waliiba pia dekoda ya televisheni, simu tatu aina ya Nokia, saa tatu, kompyuta ndogo na mkufu wa dhahabu, vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni nane.


Washtakiwa walikana mashitaka na kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 23, mwaka huu. Washtakiwa walirudishwa rumande baada ya kukosa dhamana.


Wakati huo huo, Hamza Athumani (37) na Hindu Majala (31), walifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za wizi wa kutumia silaha, wakidaiwa kuiba vito vya dhahabu na simu moja, vyenye thamani ya Sh milioni 17, mali ya Fatma Ally. Ilidaiwa kuwa walitenda kosa hilo Juni 11 mwaka huu katika makutano ya Mtaa wa Narung’ombe na Muheza wilayani Ilala.


Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents