Habari

Mwanamfalme wa Saudia Arabia ashutumiwa kudukua simu ya tajiri namba moja duniani

Mwanamfalme wa Saudia Arabia ashutumiwa kudukua simu ya tajiri namba moja duniani

Mwanamfalme wa Saudia Mohammed Bin Salman ameshutumiwa kwa kushiriki katika udukuzi wa simu ya mwanzilishi wa kampuni ya Amazon na mmiliki wa gazeti la The Washington Post Jeff Bezos.

Madai hayo ya udukuzi yalifanyika miezi mitano kabla ya kifo cha mwandish wa The Washinton POst na rais wa Saudia Jamal Khashoggi ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa ufalme huo .

Simu ya bwana Bezos ilidukuliwa baada ya kupokea ujumbe wa WhatsApp mnamo mwezi Mei 2018 ambao ulitumwa kutoka kwa akaunti ya kibinfasi ya mwanamfalme huyo, kulingana na gazeti la The Guradian ambalo lilichapisha habari hiyo.

Uchunguzi kuhusu ukiukaji huo wa data ulibaini kwamba simu ya bilionea huyo ilianza kugawa idadi kubwa ya data baada ya kupokea kifurishi cha kanda ya video.

Wataalam wa haki za kibinadamu wametaka uchunguzi wa mara moja kufanywa kuhusiana na madai kwamba mwanamfalme wa Saudia aliidukua simu ya mmiliki wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos.

Wanasema kwamba Mohammed bin Salman pia anafaa kuchunguzwa kwa kuendelea kuwalenga moja kwa moja watu anaowaona kuwa wapinzani wake.

Ujumbe kutoka kwa nambari ya simu inayotumika na mwanamfalme huyo imehusishwa na uingiliaji wa data ya bwana Bezos.

Ubalozi wa Saudia nchini Marekani umekana habari hiyo walioidai kuwa upuuzi.

Je udukuzi huo ulifanyika vipi?

Wataalam hao wa UN walisema kwamba uchunguzi wa kimaabara wa simu ya iPhone ya bwana Bezos ulibaini wazi kwamba simu yake iliingiliwa tarehe mosi mwezi Mei 2018 kupitia faili ya video iliotumwa kwake kutoka kwa akaunti ya mtandao wa WhatsApp ambayo inatumika binafsi na Mohammed bin Salman.

Wachunguzi wanasema kwamba walipata ushahidi unaohusisha Saudia na udukuzi wa ujumbe wa bwana Jeff Bezos kwa mpenzi wake Lauren SanchezWachunguzi wanasema kwamba walipata ushahidi unaohusisha Saudia na udukuzi wa ujumbe wa bwana Jeff Bezos kwa mpenzi wake Lauren Sanchez

Mwanamfalme huyo alibadilishana nambari za simu mwezi mmoja mapema na saa chache kabla ya kuwasili kwa kifurushi hicho cha kanda ya video kabla data ya simu ya bwana Bezos kuingiliwa.

Wachanganuzi hao wanasema kwamba mwanamfalme huyo baadaye alituma ujumbe wa WhatsApp kwa simu ya bwana Bezos ambapo alifichua habari za kibinfasi na zile za siri kuhusu maisha ya kibinfasi ya bwana Bezos.

Habari za kibinfasi baadaye zilifichuliwa kwa jarida la Marekani , National Enquirer.

Mwezi Februari 2019 bwana Bezos alilishutumu gazeti hilo kwa kutaka kumlaghai baada ya kuchapisha ujumbe kati yake na mpeniz wake , aliyekuwa mtangazi wa runinga ya Fox Luuren Sanchez.

Mwezi mmoja baadaye yeye na MacKenzie Bezos mkewe na miaka 25 , walitangaza kwamba walipanga kutalakakiana baada ya kuetngena kwa muda mrefu.

Ni nini walichosema wataalam hao?

Lakini mtaalama huru wa Umoja wa mataifa Agnes Callamard, mbaye ni mjumbe maalum wa mauaji na kiholela na David Kaye mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza walisema kwamba kuhusika kwa mwanamfalme huyo kunahitaji kuchunguzwa.

Uhusiano kati ya Saudia na bwana Bezos – ambaye pia anamiliki gazeti la The washington Post uliharibika zaidi baada ya Jamal Khashoggi , mkosoaji mkuu wa serikali ya Saudia na mmoja wa wafanyakazi wa gazeti hilo kuuaawa katika ubalozi wa Saudi mjini Istanbul 2018.

Jamal Khashoggi 2014Kulingana na Umoja wa Mataifa Khashoggi aliuawa katika mauaji ya kiholela yaliopangwa

Mauaji hayo yalifanyika miezi kadhaa baada ya udukuzi huo kufanyika.

Katika taarifa , bi Callamard na bwana Kaye walisema: Habari tulizopokea zinaonyesha uwezekano wa mwanamfalme kuhusika katika upelelezi wa bwana Bezos, katika juhudi za kulishawishi au kulinyamazisha gazeti la The Washington Post kuhusu habari za Saudia.

Ripoti hiyo ilisema kwamba madai hayo yalithibitisha ripoti nyengine kuhusu upelelezi wa wapinzani wengine na wale walio na umuhimu mkubwa wa kimkakati kwa mamlaka hiyo ya Saudia.

Wataalam hao walihusisha kisa hicho na kile cha mauaji ya Khashoggi, wakisema kuwa simu ya rmwanahabari huyo wa Washington Post ilidukuliwa wakati mmoja na ile ya bwana Bezos.

Walisema kwamba kumekuwa na kampeni ya kisiri ya mtandaoni dhidi ya bwana Bezos na Amazon ,ikimlenga yeye binafsi kama mmiliki wa gazeti la The Washington Post.

Taarifa hiyo pia ilitaka “udhibiti mkali” wa “, uuzaji na utumiaji wa kirusi cha spyware”.

Je raia wa Saudia na Bezos wamesemaje?

Akaunti ya twitter ya ubalozi wa Saudia nchini Marekani ilikana moja kwa moja madai hayo dhidi ya mwanamfalme huyo.

”Tunaitisha uchunguzi kuhusu madai hayo ili tuweze kujua ukweli”, ubalozi huo ulisema.

Bwana Bezos hajatoa tamko lolote kuhusu matamshi hayo ya wataalam wa UN, lakini alituma picha ya yeye na mchumba wa Khashoggi pamoja na alama ya reli #Jamal:

Presentational grey line
Chapa ya WhatsApp

Jeff Bezos, ambaye ndiye mwanzilishi wa kampuni ya Amazon na mtu tajiri zaidi duniani alikuwa na uhusiano wa kirafiki na mwanamfalme Bin Salman na maslahi ya kibiashara nchini Saudia kabla ya mauaji ya Khashoggi.

Lakini uhusiano wao ulidhoofika baada ya Bezos kuunga mkono gazeti lake ambalo lilikuwa likiishutumu Saudia kuhusu habari za mauaji hayo.

Mwandishi wa Oslo na mwanaharakati Iyad el Baghdad, ambaye alikuwa rafiki wa Khashoggi anasema kwamba udukuzi wa simu ya mtu tajiri duniani unatuma ujumbe kwa wakosoaji wa ufalme huo wa Saudia mjini Riyadh.

Aliandika: Iwapo mtu tajiri zaidi anaweza ‘kudukuliwa na hata kulaghaiwa , basi ni nani aliyesalama?

Presentational grey line

Malumbano kati ya Bezos na Saudia

  • Jun 2017 – Jamal Khashoggi atoroka Saudi Arabia na kwenda katika maficho ya kibinafsi nchini Marekani
  • Sept 2017 – Khashoggi anaanza kuliandikia gazeti la The Washington Post , akiikosa sera za Mohammed bin Salman
  • Apr 2018 – Bwana Bezos ahudhuria chakula cha jioni na mwanamfalme huyo na wanabadilshana nambari za simu
  • 1 Mei 2018 – Bwana Bezos anapokea kifurushi cha kanda ya video kilichodaiwa kutumwa na akaunti ya kibinafsi ya WhatsApp ya simu ya mwanamfalme wa Saudia . data ya simu ya Bwana Bezos yavuja.
  • 2 Okt 2018 – Jamal Khashoggi auwawa ndani ya ubalozi wa Saudia mjini Istanbul
  • Nov 2018-Feb 2019 – Mwanamfalme Mohammed amtumia Bezos ujumbe wa WhatsApp akimfichulia habari za kibinafsi na nyengine za siri kuhusu maisha ya kibinafsi ya Bezos.
  • Jan 2019 – Gazeti la National Enquirer lachapisha ugunduzi kuhusu mpenzi wa kando wa bwana Bezos Lauren Sanchez
  • Feb 2019 – Bwana Bezos alishutumu gazeti la National Enquirer kwa kujaribu kumlaghai . Mchapishaji wake anasema kwamba alifuata sheria
  • Jan 2020 – Wataalam wa UN wataka uchunguzi kufanywa dhidi ya mwanamfalme huyu.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents