Tupo Nawe

Mwanamieleka John Cena awatangazia habari mbaya mashabiki wake “Bado nahitajika ila naona umri unaniacha”

Mwanamieleka maarufu nchini Marekani, John Cena amesema kuwa kwa sasa anafikiria kustaafu kucheza mchezo huo kwa kile alichodai kuwa umri unamtupa mkono.

John Cena katikati kwenye picha.

Cena mwenye miaka 42, akiongea na mtandao wa TMZ, John Cena amesema kuwa amefikiria hivyo baada ya kutazama mchezo kati ya  The Undertaker na Bill Goldberg mchezo uliopigwa Ijumaa iliyopita nchini Saudi Arabia.

Mchezo huo kati ya Taker na Goldberg uliwaboa mashabiki wengi wa mieleka baada ya mahasimu hao kuonekana wote wawili kuchoka mwanzoni mwa pambano hilo.

John Cena amesema ameshangazwa na wanamieleka hao kucheza chini ya kiwango na anajiona na yeye anaelekea huko, hivyo haoni sababu ya kuendelea kucheza mchezo huo siku za usoni.

“Nadhani nafikiria kuachana na mchezo huu siku za hivi karibuni, Ingawaje bado mashabiki wananihitaji. Unajua umri unaenda mbio sana, Nilivyoangalia pambano lile *Taker vs Goldberg* niliona namna walivyokuwa wanapoteza muda kila mmoja alichoka uwanjani ile ni dalili tosha huu sio muda wetu.” amesema John Cena .

Hata hivyo, John Cena hajataja rasmi ni lini atatangaza kustaafu, lakini kutokana na majeraha yanayomuandama mara kwa mara huenda siku sio nyingi akatangaza adhma hiyo.

Kwa upande mwingine, John Cena amemshukuru Vin Diesel kwa kumshirikisha kwenye series ijayo ya Fast and Furious franchise.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW