Soka saa 24!

Mwanamitindo,Katarina ang’atwa na papa akipiga nao picha (+Video+Picha)

Kisiwa cha Exuma nchini Bahamas kina umaarufu mkubwa wa kuwa na michanga meupe iliyopo ufukweni mwa bahari , maji masafi na maeneo mengi ya kuvutia.

Hivyo basi mwanamitindo Katarina Zarutskie alipozuru huko pamoja na mpenzi wake, mwezi uliopita alikuwa na ari ya kutumia maeneo mazuri ya fukwe hiyo ya bahari.

Katarina Zarutskie

Baada ya chakula cha mchana na familia katika eneo linalojulikana kama Staniel Cay, Katarina aliwaona watu waliyokuwa wakiogelea karibu na papa mchanga katika eneo moja.

Licha ya familia ya mpenzi wake kuwa na wasiwasi, alikuwa yuko tayari kuingia katika maji hayo ili kupiga nao picha.

Katarina Zarutskie anaonekana akitaabika majini

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye anatarajia kuanza mafunzi ya shahada mbili za uuguzi na biashara mjini Miami siyo mgeni wa maswala ya bahari baada ya kukuwa akifanya michezo ya baharini nyumbani kwao huko mjini California.

Katarina Zarutskie akishikilia mkono wake baada ya kung'atwa

”Kutokana na ufahamu wangu wa kuteleza majini na kuogelea chini ya maji najua kwamba papa wachanga huwa salama. Nimeona watu wengi wakipiga picha nao katika mtandao wa Instagram,” aliambia BBC .

Katarina ameongeza kuwa baada ya dakika chache za uwepo wake maeneo hayo raia mmoja wa eneo hilo alimshawishi kuogelea kwenye maji hayo huku akiangalia juu.

”Wakati huo watu walikuwa wameanza kupiga picha , nilipokuwa nikilala kwenye maji kwa kuangalia juu nilihisi kitu kimenivuta chini”.

Samaki huyo amekuwa kivutio cha watalii, akizurura katika gati mbali mbali na kuonekana katika maelfu ya picha zilizosambazwa katika mitandao.

Jeraha la meno

Maeneo aliyong’atwa mrembo huyo, Katarina Zarutskie 

Mpenzi wake alikuwa akimpiga picha Katarina wakati huo na kwa bahati nzuri akapata kisa chote katika kamera yake.

Papa huyo alimzuilia chini ya maji kwa sekunde chache kabla ya kuamua kuondoa kiganja chake cha mkono katika mdomo wake.

Picha hizo zinamuonyesha akifunika jereha hilo na kuinua mkono wake katika juhudi za kuzuia damu kuenea katika maji .

“Wakati huo mwili wangu ulikuwa na wasiwasi mwingi na hatua ya pekee ni kujiondoa katika hali hiyo, lakini nilitulia. Nadhani iwapo mtu angepiga kelele na kuinua mikono akitafuta usaidizi hali ingebadilika”.

Katarina alilazimika kushonwa na kupewa dawa na bado ana vipande vya meno vya papa huyo vilivyosalia katika kidonda hicho.

Jeraha hilo la meno litawacha kovu baya , lakini mwanamitindo huyo alisema kwamba anahisi amebarikiwa tukio hilo halikuwa baya sana.

Tangu habari yake kuchapishwa katika vyombo vya habari vya Marekani , Katarina amepokea maelfu ya mashabiki katika mtandao ikiwemo waliyo mshutumu mrembo huyo kukusudia tukio hilo.

Mwanamitindo huyo hakupanga kuposti picha hizo katika mitandao yake ya kijamii hadi alipofuatwa na waandishi kuhusu uzoefu wake wiki hii.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW