Habari

‘Nimeungua mara tatu, nimefanyiwa upasuaji mara 4’-Aeleza mrembo aliyepitia magumu 2016

Ni Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 aitwaye Julie S.-Future alipitia mateso makubwa sana na ya kutisha mwaka 2016 kwa kuungua Maeneo makubwa katika ngozi yake
Julie alitumia wiki 4 katika kutibiwa hospitalini na alifanyiwa upasuaji mara 4.

Mwanadada huyo ali hadithia stori yake kwa kusema hivi
“Ilikuwa ni Julai 21 ya mwaka 2016 ambapo nilikuwa muhudumu katika klabu moja hivi. chakula kilikuwa kikiandaliwa chini ya hema karibu na mlango wa jikoni wa klabu hiyo. Usiku huo kulikuwa na umati wa wateja katima hema hilo. Wateja wawili wakapingia kwenye mzozo na mmoja akatoa bunduki na kuanza kumimina risasi.
Kila mtu akageukia njia anayo ijua nakukimbia kulikuwa na majiko mbalimbali ya umeme yaliyokuwa na mafuta.
Muda mfupi baadaYe mafuta yakaanzaa kuruka kila mahali na yalinirukia mgongoni kwenye nguo yangu na kuanza kuteketeza ngozi yangu. Katika hatua hiyo mimi niliingia ndani ya klabu na kusubiria risasi kuacha kupigwa.
Nilipofika hospitali dakika thelathini baadaye waliniondoa nguo na wakasema itakuwa vigumu kwa mimi kupata matibabu hapo kwa sababu hawana vifaa vya kutosha. Waliwezatu kunipa mifuko kadhaa ya morphine na kuhamishiwa Center Burn na ndo nilipo tumia wiki 4 kutibiwa nakufanyiwa upasuaji mara nne. Kiukweli nilipatwa na maumivu makali mno”

Julie aliongezea kwa kusema kwamba “Wakati nilivyotolewa hospitali nilipatiwa daktari wa mwili kwa muda wa miezi mitatu ili kurejesha mwenendo wangu. Muda huo nilijawa na huzuni na mahangaiko na nilipata shida kukubali kwamba hii ndiyo ngozi yangu mpya. Nilikuwa na umri wa miaka 22 na niliona kama kutokuwa na ngozingozi kamili ilikuwa kama ninalipishwa dhambi zangu. Nilikuwa nikifanya ibada kwa sana na kujifajiri mwenyewe mpaka kufikia hatua hii niliopo leo. Kwa sasa nina umri wa miaka 24 na nipo tayari kwa ajili kupambana na dunia. Kamwe katika maisha yangu sikudhani kama ningefika hapa nilipo na ninadhani nikwaajili ya kujipenda mimi mwenyewe.”

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents