Soka saa 24!

Mwanamke alipwa zaidi ya bilioni 4 za kitanzania, kwa kupewa majibu yasiyo sahihi katika kipimo cha saratani ya uzazi

Mwanamke alipwa zaidi ya bilioni 4 za kitanzania, kwa kupewa majibu yasiyo sahihi katika kipimo cha saratani ya uzazi

Mwanamke anayeuguza saratani ya amezawadiwa £1.8m kama fidia ya madhara aliyoyapata kwa kupewa matokeo yasiyo sahihi ya kipimo cha saratani ya mfuko wa uzazi na kushindwa kumwambia ukweli juu ya vipimo sahihi. Ruth Morrissey na mumewe Paul, kutoka eneo la Monaleen, Kounti ya Limerick, nchini Uingereza waliishtaki maabara ya HSE na maabara nyingine mbili – MedLab Pathology Limited na Quest Diagnostics kwa kuwapatia matokeo ya kipimo cha saratani ya mfuko wa uzazi- Papsmear kwa lugha ya kitalaamu.

Kwa mujibu wa BBC. Hii ni kesi ya kwanza ya aina hii kusikilizwa kikamilifu na kutolewa hukumu na mahakama ya juu ya Irland.

Bi Morrissey, mwenye umri wa miaka 37, kwa mara ya kwanza alibainika na saratani ya mfuko wa uzazi mnamo 2014.

Lakini mahakama iliambiwa kuwa hakufahamishwa kuhusu ugonjwa wake mpaka mwezi Mei mwaka jana kwamba tathmini ya vipimo vya awali vya Papspsmear ilionyesha kuwa havikutoa majibu sahihi.

Alidai kuwa kama vipimo vya 2009 na 2012 vingetathminiwa na kuripotiwa kwa usahihi angekuwa amefanikiwa kutibiwa na asingekuwa na saratani .

Bi Morrissey pia alidai kuwa angefahamu matokeo ya tathmini ya 2014 mapema , angekuwa ameomba kufanyiwa vipimo zaidi vya skani na angelifuatilia hali yake.

Bi Morrissey aliiambia mahakama kuwa hadhani kuwa kamwe angeliambiwa tathmini ya vipimo vyake vya saratani kama isingekuwa kesi ya Vicky Phelan, ambaye aliishitaki maabara ya Marekani mwaka mmoja uliopita.

Kipimo cha saratani ya mfuko wa uzazi PapsmearHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY

Huku wanawake kadhaa wakiwa pia wameweza kuzishtaki maabara kwa kutowapa vipimo sahihi vya maradhi yao na kulipwa fidia , kesi hii iliyodumu kwa muda wa sikiu 35, ni ya kwanza ya aina yake kuwahi kupewa fursa ya kusikilizwa kikamilifu na kutolewa hukumu na Mahakama ya juu zaidi.

Bi Morrissey, ambaye ana binti yake mdogo, aliiambia mahakama kuwa hakutaka kufa. Maabara ya HSE ilikiri kuwa ilikuwa na jukumu la kumuhudumia Bi Morrissey . Maabara nyingine zilikama madai yote.

Chanzo:-

https://www.bbc.com/swahili/48149957

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW