Habari

Mwanamke aliyekatazwa kutafuta ajira na mumewe amwagiwa tindikali kwa kosa la kupata kazi

Mwanamke mmoja kutoka katika wilaya ya Malwani, Mumbai nchini India amejikuta akipata kilema cha kudumu baada ya kumwagiwa tindikali usoni na mumewe siku mbili baada ya kupata ajira serikalini.

Zakira Ali Sheikh

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Zakira Ali Sheikh (26) amesema alikatazwa na mumewe ‘Roobab Ali Sheikh’ kutafuta kazi yoyote ya kuajiriwa na kuambiwa kuwa abaki tu nyumbani kwa ajili ya kulea familia na kazi ndogo ndogo.

Mwanamke huyo wakati anasimulia kisa hicho kwenye mahojiano yake na gazeti la Hindu Times la nchini India amesema mumewe alikuwa ni fundi magari na alikuwa haachi pesa ya matumizi nyumbani kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza kichwa jinsi ya kuendesha familia yao yenye watoto wawili.

Bi. Zakira ambaye tayari jicho lake moja limeshapata upofu amesema alishindwa kuvumilia hali hiyo ndipo alipoamua kupeleka maombi ya kazi kwenye kiwanda cha Serikali cha Sabuni baada ya kuona matangazo ya kazi.

Anasema baada ya siku mbili aliona jina lake kwenye mtandao kuwa amechaguliwa kuanza kazi kwenye kiwanda hicho ndipo alifanya taratibu zote na kuanza kazi bila kumjuza mumewe.

Hata hivyo aliona sio vyema kukaa kimya ndipo siku ya tatu alipoamua kumwambia mumewe usiku na kuanza kuambulia kipigo na kisha kumwagiwa tindikali usoni.

Nilipiga makelele usiku ule kwa muda wa dakika 10 lakini hakuna jirani aliyekuja kuniokoa hadi baadae kaka yangu alipokuja kuniokoa, niliumia sana nilijiona kama nakufa.“amesema Bi. Zakira .

Jeshi la polisi mjini Mumbai limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limesema tukio hilo limetokea tarehe 14 Novemba mwaka huu na tayari mtuhumiwa amekamatwa kwa mahojiano zaidi.

Kwa sasa mwanamke huyo anatibiwa katika hospitali ya Mumbai nchini humo na amewekewa mipira ya kupumulia ambapo anahitaji msaada wa Euro 29,090 sawa na Tsh milioni 76 ili aweze kukamilisha upasuaji.

Tayari mashirika binafsi yameshajitolea kumsaidia mwanamke huyo likiwemo shirika la ‘Make Love Not Scars’ kwa kumshangia dola $11,0000.

Vyanzo : Hindu Times & Daily Mail

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents