Tupo Nawe

Mwanamke amekutwa amekufa huku nyoka mwenye sumu aliyemfuga akiwa amemzunguka kwenye shingo – Video

Mwanamke amekutwa amekufa huku nyoka mwenye sumu aliyemfuga akiwa amemzunguka kwenye shingo - Video

Mwanamke mmoja amekutwa amekufa katika jimbo la Indiana nchini Marekani ahuku nyoka mwenye sumu akiwa amemzunguka katika shingo.

Laura Hurst ambaye alikuwa na umri wa miaka 36, alikutwa maiti na polisi mara baada ya kufika katika mji wa Oxford.

Nyumba hiyo ilikuwa na nyoka 140 ndani, jambo ambalo inaaminika kuwa nyumba hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kuhifadhi wanyama.

Nyoka wapatao 20 wanamilikiwa na bi Hurst ambaye alikuwa anawatembelea mara mbili kwa wiki.

Ingawa nyumba hiyo inadaiwa kuwa inamilikiwa na mkuu wa polisi katika kaunti ya Benton, Don Munson ambaye anaishi nyumba jirani.

Anasema kuwa alimkuta Hurst kwenye sakafu, gazeti la nchini humo linaripoti.

Aliliambia gazeti hilo kuwa kifo cha bi Hurst kilikuwa ni “ajali kubwa na amekuwa akionyesha ushirikiano na kila mtu”.

Kamanda polisi katika jimbo la Indiana, Kim Riley anasema kuwa mtu huyo ambaye alimkuta Hurst aliweza kuwaondoa nyoka hao shingoni lakini watu wa dharura walipofika walishindwa kumuokoa.

Bi.Hurst, alijeruhiwa na nyoka hao ingawa ni kitu ambacho alikuwa anakifanya kila wakati bila kudhurika.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW