Habari

Mwanamke India aweka rekodi kuupanda mlima Everest

Anshu Jamsenpa amekuwa mwanamke wa kwanza kuupanda mlima Everest hadi kufikia kileleni katika siku tano.

Jamsenpa ambaye ana umri wa miaka 37 ni mama wa watoto wawili, alifika kileleni mwa mlima huo Jumanne ya Mei 16 wiki iliyopita na alirejea tena chini Jumapili hii.

Mama huyo amekuwa mwanamke wa kwanza kutoka nchini India kufika katika kilele cha mlima huo.

Taarifa hizo zimefika wakati wapanda milima wapatao watatu wamefariki dunia ndani ya wiki moja akiwemo mmoja kutoka Australia alifariki akipanda mlima huo kutoka upande wa Tibet, naye raia wa Slovakia na mmoja kutoka Marekani walifariki dunia katika upande wa Nepal.

Maafisa wa uokoaji wameshindwa kumfikia mpanda milima wa nne, ambaye anatoka India, na ambaye alitoweka muda mfupi baada ya kufika kileleni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents