Habari

Mwanamke tajiri zaidi Afrika afunguliwa mashtaka ya ulaghai, Fahamu zaidi

Angola yamfungulia mashtaka ya ulaghai mwanamke tajiri barani Afrika Isabel dos Santos

Mwanamke tajiri zaidi Afrika Isabel dos Santos amefunguliwa mashtaka ya ulaghai baada ya kutuhumiwa kwa kulipora taifa hilo na waendesha mashtaka.

Mwanasheria mkuu Helder Pitta Groz alisema kwamba madai hayo yanahusiana na wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Sonangol. Watu kadhaa pia wametuhumiwa pamoja na bi dos Santos.

Bwana Pitta Groz alisema kwamba kibali cha kimataifa cha kuwakamata iwapo watakosa kujiwasilisha mbele ya mamlaka ya Angola.

“Isabel dos Santos anatuhumiwa kwa usimamizi na ufujaji wa fedha wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Sonangol hivyobasi amefungliwa mashtaka ya usimamizi mbaya wa ofisi , kutumia ushawishi wake na kughushi stakhabadhi miongoni mwa uhalifu mwengine wa kiuchumi”, bwana Pitta Gross aliambia mkutnao na wanahabari siku ya jumatano jioni.

Uchunguzi kuhusiana na usimamizi wake wa kipindi cha miezi 18 katika kampuni hiyo ya mafuta kuanzia mwezi Juni 2016 ulianzishwa baada ya mrithi wake Carlos Satumino kuelezea mamlaka kuhusu uhamishaji wa fedha usio wa kawaida .

Stakhabadhi zilivuja wwiki hii zikidai kwamba bi Dos Santos , mwana wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jose Eduardo dos Santos , alijipatia mali ya thamni ya dola bilibo 2.1 kwa kulipora taifa lake. Amekana madai hayo.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents