Habari

Mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi awa mgombea mwenza Urais uchaguzi Mkuu

Mgombea wa Urais wa chama cha Democratic Joe Biden amemtaja Seneta Kamala Harris kama mgombea mwenza-akiwa ni mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kugombea wadhifa huo.

Kamala Harris standing in front of an American flag

Kamala ambaye wakati mmoja alikua hasimu wake katika mchuano wa kuwania urais, ni seneta wa California mwenye asili ya India-na Jamaica ambaye kwa muda mrefu amekua akichukuliwa kama mgombea wa nafasi ya pili baada ya Biden.

Mwanasheria huyo mkuu wa zamani wa California amekua akitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi katika polisi ya Marekani wakati wa maandamano ya kitaifa ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Bwana Biden atakabiliana na Rais Donald Trump katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 3 Novemba mwaka huu.

Bi Harris anasema wakati wote amekuwa akijivunia utambulisho wake na anajieleza binafsi kama ”Mmarekani”.

Mwaka 2019, aliliambia jarida la Washington Post kwamba wanasiasa hawapaswi kupewa nafasi etu kwasababu ya rangi au wanakotoka.” Nilikua nataka kusema hivi: Mimi ni mimi niliovyo. Nina uwezo . Unaweza kuhitaji kunielewa, lakini niko sawa na jinsi nilivyo ,” alisema.An undated handout photo made available by the Biden Harris Campaign

Katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House Jumanne, Bwana Trump , ambaye ni Mrepuplican , alimuelezea Bi Harris kama ” Mtu ambaye wa kwanza ninayeweza kumchukua”

Bi Harris atakua na mjadahalo na mgombea mwenza wa Trump, Mkamu wa rais Mike Pence, tarehe 7 Oktoba Salt Lake City, Utah.

Ni wanawake wengine wawili tu ambao wamewahi kugombea wa viti vya Makamu wa Rais nchini Marekani -Sarah Palin kutoka chama cha Republican mwaka 2008 na Geraldine Ferraro wa Democrats mwaka 1984. Hatahivyo hakuna mmoja wao aliyeweza kufika White House.

Mwnamke mwenye asili nyeusi hajawahi kuteuliwa kwa tiketi ya urais na vyama vyote viwili. Pia hakuna mwanamke aliyewahi kushinda kiti cha urais nchini Marekani Biden na Harris wamesema nini?

Bwana Biden alituma tweet akisema kwamba amekua na “heshima kubwa” kumtaja Bi Harris kama mtu wake nambari mbili.

Biden na Harris wamesema nini?

Alimuelezea kama “mpiganaji asiye na uoga kwa mwanaume mdogo, na mmoja wa wahudumu bora wa umma “.

Alielezea jinsi alivyofanya kazi karibu na marekemu mtoto wake wa kiume, Beau, alipokua Mwanasheria Mkuu wa California.

“Nilishuhudia walipochukua benki kubwa , wakawainua wafanyakazi, wakawalinda wanawake na watoto dhidi ya unyanyasaji ,” he tweeted.

“Nilijjivunia sana wakati huo, najivunia sasa kuwa nae kama mwenzangu katika kampeni hii .”Joe Biden akizungumza na Kamala Harris kupilitia link ya video link, ilitolewa na mpiga picha rasmi wa kampeini yake

Bw Biden akimfahamisha Bi Harris kwamba atakua mgombea mwenzake siku ya Jumanne

Baadae Bi Harris alitweet Bwana Biden “anaweza kuunganisha watu wa Marekanikwasababu ameishi miaka yake akipipambana kwa ajili yetu . Na kama rais, atajenga Marekani inayotufaa.

“Nina heshima kujiunga nae kama mtu aliyeteuliwa na chama kugombea kiti cha Makamu wa Rais na kufanya yapasayo kumfanya awe Amir jeshi .”

Kampeni ya Chama ilitangaza kuwa Bwana Biden na Bi Harris watatoa hotuba zao katika Wilmington, Delaware, Jumatano juu ya “jinsi watakavyofanya kazi kwa pamoja kurejesha moyo ya taifa na kupigania familia zinazofanya kazi kuendeleza mbele taifa “.

Bwana Biden aliahidi mwezi Machi kwamba atamtaja mwanamke kugombea wadhifa wa Makamu wa rais. Alikabiliwa na miito mingi kumteua mwanamke mweusi katika miezi ya hivi karibuni wakati taifa lilipokua likikumbwa na maandamano ya kijamii juu ya ukatili wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi.

Kamala Harris ni nani?

Bi Harris mwenye umri wa miaka 55, aliondoka kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais mwezi Disemaba baada ya kutofanikiwa kushinda katika mchuano wa uteuzi wa kiti cha urais wa chama cha Democratic.

Akikabiliana mara kwa mara na Bwana Biden wakati wa midahalo ya chaguzi za awali , ambapo alikosoa jinsi Biden alivyosifu mahusiano ya ”kiraia” ya kikazi aliyokuwa nayo na seneta wa zamani ambaye alipendelea ubaguzi wa rangi.

Alizaliwa katika Oakland, California, na wazazi wahamiaji :Mamayake alikua ni muhindi na baba yake Mjamaica.

Alisoma hadi Chuo Kikuu cha Howard , ambacho ni moja ya vyuo maarufu walivyosomea watu weusi kihistoria. Alielezea muda wake chuoni k= hapo kama moja ya maeneo yaliyojenga maisha yake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents