Burudani

Mwanamuziki akamatwa Saudia kwa kosa la kucheza ‘dabbing’ (Video)

By  | 

Mwanamuziki maarufu amekamatwa kwa kucheza ”dabbing” wakati wa tamasha kusini magharibi mwa Saudia.

Abdallah Al Shahani, mtangazaji wa runinga, muigizaji na raia wa Saudia alikuwa akionyesha miondoko hiyo ya densi ya dabbing ambayo inashirikisha mcheza densi kuingiza kichwa chake chini mkono katika tamasha la muziki katika mji wa Taif wikendi iliopita.

Dabbing imepigwa marufuku katika taifa hilo la kihafidhina ambapo utawala unaifananisha na utamaduni wa utumizi wa mihadarati.

Kanda ya video ya densi hiyo ya bwana Al Shahani ilikuwa maarufu katika mitandao ya kijamii na maelfu wametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuhusu kisa hicho.

Inadaiwa kuwa dabbing inatoka katika muziki wa Hip- Hop katika jimbo la Atlanta, Georgia, Marekani, takriban miaka miwili iliopita lakini ikapata umaarufu baada ya watu maarufu , wanariadha na wanasiasa

Waziri wa maswala ya ndani anayehusika na kukabiliana na mihadarati nchini Saudia hivi majuzi alipiga marufuku densi hiyo kwa kuwa wanaifananisha na watumiaji wa bangi.

Chapisho lililowekwa na wizara hiyo linawaonya raia kuhusu hatari yake katika vijana na jamii na inaonya dhidi ya kuiiga .

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments