Habari

Mwanamuziki nguli wa Kenya, Benga Joseph Kamaru afariki dunia

Mwanamuziki nguli raia wa Kenya, Benga Joseph Kamaru amefariki dunia hapo jana siku ya Jumatano katika hospitali ya MP Shah (MP Shah hospital) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mzee Kamaru amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 huku akikumbukwa zaidi miaka ya 1980 kwa vibao vyake vingi mashuhuri vikiwemo ‘Tiga Kuhenia Igoti’ (Usihadae mahakama), na ‘Muhiki wa Mikosi’ alivyokuw akiimba kwa lugha ya Kikuyu.

Rais Uhuru Kenyatta na viongozi mbalimbali wa Kenya wameonyesha kuguswa na kifo chake na kuposti ujumbe mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter.

Kamaru aliyezaliwa mwaka 1939 na kufariki dunia hapo jana Oktoba 3, 2018 anakadiriwa kuwa na nyimbo zaidi ya nyimbo 2000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents