Mwanasayansi nguli Stephen Hawking afariki dunia

Mwanasayansi nguli na mnajimu, Stephen Hawking, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.


 Stephen Hawking

Tukio la kifo hicho kimetangazwa na familia yake ambapo wamesema, Profesa Hawking amefariki Jumatano asubuhi.

Katika taarifa hiyo ambayo imetolewa na watoto wake Lucy, Robert na Tim inasema: “Tunahuzunika sana baba yetu mpendwa amefariki leo. Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi.”

Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada yake kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.

Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu.

Nyakati za mwisho za maisha yake, alikuwa hawezi kuzungumza ila kwa kutumia kifaa cha kufasiri mawazo yake na kuyageuza kuwa sauti.

Wakati huo huo mwezi Novemba mwaka 2016 Prof. Hawking alipoongea kwenye chuo kikuu cha Oxford alisema, kutokana na utafiti wake wa kisayansi aliowahi kuufanya, binadamu hawatoweza tena kuishi katika ardhi ya dunia kwa miaka 1,000 mingine, na chanzo kitakuwa yale yale, mabadiliko ya tabia nchi, mabomu na roboti.

Hawking alisema njia pekee itakayotupa maisha zaidi, ni kuhama kwenye dunia hii na kwenda kutengeneza makoloni kwenye sayari zingine.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW