Habari

Mwanasheria Albert Msando afafanua sakata la Shilole na Uchebe nani mwenye kosa na sheria inasemaje (+Video)

Tukio la kupigwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva Shilole alimaarufu Shishi limevuta hisia za watu wengi sana na kumekuwa na mijadala mingi sana mitandaoni wengi wakimtetea Shilole huku wengine wakimtetea Uchebe bila kujua vifungu vya sheria vinasemaje.

Mmoja ya wanasheria maarufu sana na wakubw ahapa nchini Albert Msando ametolea ufafanuzi kosa kama alilofanyiwa Shilole, kupitia ukurasa wake wa Instagrama ameandika haya:-

@policetanzania nimemsikia anayeitwa Uchebe kwenye @cloudstv kwamba hizi picha ni za zamani. Hivyo kimsingi amekubali kwamba alimpiga @officialshilole ila zamani. MIMI NIMESIKILIZA NA KUSOMA ALICHOSEMA KAMA MNAHITAJI SHAHIDI. Kosa la jinai halina muda. Hata kama lilifanyika miaka ya 1980! Kama lilikuwa ni kosa kisheria basi aliyetenda lazima adhabu inamuhusu. Nitashangaa kama ‘upelelezi bado unaendelea’ mpaka ikifika mwezi wa nane. Ni vyema muda akitoka jela akute kiberiti kinauzwa elfu 15 na box spanner inauzwa kama laki 6 hivi. Tuone gereji atakuwa na spanner ngapi na ghetto atawasha jiko la mchina na nini. #UteteziWaKujifunga #IncriminatingEvidence @auntsadaka @joycekiriasuperwoman

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents