Mwanasheria amtolea uvivu Waziri Mkuu

“Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imetakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria watuhumiwa wa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA)”
– Tundu Lissu



Tundu Lissu


 


Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imetakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria watuhumiwa wa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu ya Tanzania BOT kwa kuwa sheria hazikutungwa kwa ajili ya masikini tu bali hata wao zinawahusu.



Hayo yalisemwa na mwanasheria wa haki za binadamu, Tundu Lissu wakati akiijadili kauli ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda aliyoitoa mjini Dodoma kuwa utajiri wa baadhi za watuhumiwa katika akaunti ya EPA ni moja ya vikwazo vinavyoweza kuifanya serikali kushindwa kuwafikisha mahakamani.



Hii sio kweli kuwa Serikali inashindwa kuwafikisha mahakamani kwa sababu ya utajiri, ni sababu ambazo hazina msingi wowote kwani sheria hazikutungwa kwa ajili ya kuwakamua watu masikini peke yao,”.


Alieongeza bwana Lissu kwa kusema kuwa kauli hiyo haikupaswa kutolewa na Waziri Mkuu kwani sheria haielezi kuwa mtuhumiwa arejeshe mali alizoiba kwanza ndipo akamatwe na kushitakiwa.



“Ni dhahiri inaonesha kuwa sheria ni kwa ajili ya kuwabana masikini tu, Pinda hakutakiwa kutoa kauli kama hiyo. Inaonyesha watuhumiwa ni marafiki zao na kama hiyo ndiyo ilikuwa mbinu ya Serikali Waziri Mkuu Pinda hakupaswa kuieleza kwenye vyombo vya habari. “Kama hiyo ndiyo mbinu ni kwa nini awatangazie?” alihoji.



Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa, amesema kauli ya Pinda inadhihirisha kuwa watuhumiwa wa ufisadi ni vigogo.



“Mimi naamini kuwa vigogo wenyewe wanahusika kwa asilimia kubwa sana hivyo serikali ina hofia kuwa makamouni 22 yaliyotajwa iwapo yatafikishwa mahakamani yanaweza kufichua mambo mengi sana” alisema Dr Slaa amabye aliongeza kwa kudai kuwa anaamini pia fedha kibao zimetumika kwenye uchaguzi mkuu hivyo inaogopa kupata fedhea kubwa kwa wananchi.


 


Dk. Slaa amesema kama Serikali ingekuwa na nia ya dhati ingekuwa tayari imeeleza alipo aliyekuwa Gavana wa BOT bwana Daud Balali, tangu wananchi walipoanza kupiga kelele.


 


Amesema wao walitarajia kuwa Serikali itaanza kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuidhinisha fedha hizo kwa sababu wapo na wanajulikana.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents