Mwanasheria Mkuu wa Kenya ang’atuka

Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Prof. Githu Muigai amejiuzulu baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa miaka sita na nusu.

Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Prof. Muigai kwa kutumikia nafasi hiyo na yake itachukuliwa na jaji Paul Kihara. Kupitia ukurasa wake wa twitter Rais Kenyatta amethibutsha kujiuluzu wa Prof Githu.

“Nimepokea kwa majuto uamuzi wa mwanasheria mkuu Githu Muigai. Namshukuru kwa huduma yake katika kipindi cha miaka sita na nusu. Nimemteua jaji Paul Kiharara Kariuki” ameandika Rais Kenyatta.

Kabla ya uteuzi wake kuwa mwanasheria Mkuu Prof. Muigia alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya mawakili ya Mohammed Muigai na amekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW