Habari

Mwanasiasa huyu mkubwa nchini Kenya afikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji ya Mwanafunzi

Mwanasiasa huyu mkubwa nchini Kenya afikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji ya Mwanafunzi

Mwansiasa mkuu nchini Kenya leo amefikishwa mahakamani katika mji mkuu Nairobi kwa mashtaka ya kusaidia na kupanga mauaji. Gavana wa jimbo la Migori nchini Kenya Okoth Obado amesomewa mashtaka katika kesi ya mauji ya mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu , Sharon Atieno. Obado amekana mashtaka na mahakama imeamuru arudishwe rumande mpaka kesho Jumanne ambapo ombi lake la kutaka kuachiwa kwa dhamana litasikizwa.

Obado akiwa na wenzake wanadaiwa kumuua kikatili mwanafunzi huyo.

Kwa mujibu wa BBC, Miongoni mwa waliofika mahakamani asubuhi hii ni pamoja na mamaake Sharon Otieno, Melida Auma.Washukiwa wengine waliokamatwa katika kesi hiyo ni pamoja na msaidizi binafsi wa Gavana Obado Michael Oyamo, na afisa anayeaminika kumiliki gari lililotumika kumteka Sharon. Polisi ilimkamata Gavana Obado siku ya Ijumaa wakati uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kifo cha Sharon Otieno.

Katika siku za nyuma, Obado amekanusha madai ya kuhusika na mauaji ya mwanafunzi huyo ambaye inasadikiwa alikuwa mpenzi wake. Wiki mbili zilizopita, Obado aliwaambia polisi mjini Kisumu kwamba yeye binafsi angelipenda kuwajua wauaji wa Sharon ni kina nani. Wakili wake Obado, Cliff Ombeta anasema mteja wake hana hatia na kwamba amewaeleza polisi kila kitu alichofahamu kuhusiana na kesi hiyo.

Mtaalamu mkuu wa upasuaji wa maiti Kenya Johansen Oduor, baada ya kuuchunguza mwili wa marehemu, alisema huenda Sharon Otieno alifariki kutokana na kuvuja damu sana. Alikuwa amedungwa kisu mara nane. Mwili huo pia ulikuwa na alama za kukabwa shingoni, na alama nyingine zinazoashiria kwamba alijaribu kujiokoa. Dkt Oduor alisema kuna uwezekano kwamba Sharon alibakwa. Kesi ingali inaedelea mahakamani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents