Habari

Mwanasiasa wa upinzani DR Congo, Jean pierre Bembe arudi nyumbani

Mwanasisa maarufu wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jean pierre Bembe amerejea rasmi nyumbani baada ya kukaa miezi kumi ugenini.

Jean Pierre bemba akipokewa katika uwanja wa ndege Kinshasa na mpinzani Martin Fayulu - mgombea urais wa mwaka jana kupitia muungano wa Lamuka

Bemba alirudi Congo hapo jana kutoka Brussels Ubelgiji katika ndege binafsi na kupokewa na umati wa watu waliokusanyika Kinshasa kumlaki.

Washirika wake Bemba anasema amerudi rasmi nchini kutoa usaidizi kwa mpinzani Martin Fayulu ambaye anasisitiza kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Ni ziara ya pili ya mwanasisia huyo nchini DRC baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC baada ya kutumikia kifungo cha miaka kumi gerezani.

Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa Mbelechi Msochi anasema alihutubia kwa mara ya kwanza umati wa watu uliokusanyika na kueleza raia kile ambacho upinzani unadai ndio ukweli kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu huo,

‘Mahakama ya katiba inapaswa kuimarisha demokrasi nchini mwetu, badala yake imekuwa kama saratani inayoharibu taasisi zetu. Mmeona jinsi bunge letu limekuwana watu ambao hawakuchaguliwa ndio wamelitawala… hiyo inachafua jina la nchi yetu ugenini. Sio viongozi tu walio na haki ya kujenga nyumba’.

Bemba anapanga kusalia nchini Congo kwa muda mrefu katika kuongoza mfululizo wa maandamano aliyopanga kwa lengo la kudai haki ya uchaguzi huo.

Bemba alirudi Congo kuonesha azma ya kutaka kugombea katika uchaguzi wa mwaka jana lakini ombi lake lilitupiliwa mbali na tume huru ya uchaguzi ya DRC.

Alirudi Ubelgiji na kutangaza kuungana na Moise katumbi mgombea mwingine wa upinzani, pamoja na Martin Fayulu kupitia muunganowa Lamuka.

Wafuasi wakimsubiri Bemba awasili mjini Kinshasa JumapiliWafuasi wakimsubiri Bemba awasili mjini Kinshasa Jumapili

Umati uliokusanyika mara hii ni mdogo ukilinganishwana uliokuwepo wakati Bemba aliporudi Congo kwa mara ya kwanza kutoka uhamishoni mnamo Agosti mwaka jana baada ya kuishi kwa zaidi ya muongo mmoja nje ya nchi hiyo.

Kiongozi mwenza wa upinzani Moise Katumbi alirudi kutoka uhamishoni mwezi mmoja uliopita.

Bemba aligombea urais dhidi ya rais Joseph Kabila mnamo 2006 na alishindwa.

Alikaa kwa miaka 10 katika mahakama ya ICC kwa uhalifu uliotekelezwa na wanajeshi wake katika Jamhuri ya Afrika ya kati kabla ya kuondoshewa mashtaka na hatimaye kuachiwa huru baada ya kukata rufaa.

Anarudi nchini Congo wakati rais Tshisekedi ameingia katika makubaliano ya serikali ya muungano na kiongozi aliyemtangulia Kabila, ambaye ana uwingi bungeni.

Jean Pierre Bemba amerudi nyumbani leo, baada ya kukaa kwa takribani muongo mmoja akiwa kifungoni na nje ya nchi ya Kongo.Jean Pierre Bemba alirudi nyumbani Agosti mosi 2018 baada ya kukaa kwa takribani muongo mmoja akiwa kifungoni na nje ya nchi ya Congo.

Mambo Makuu kumhusu Jean Pierre Bemba

Jean-Pierre Bemba alizaliwa mwaka 1962 kwenye mkoa wa kaskazinia magharibi wa Equateur, Baba yake, bilionea Bemba Saolona alikuwa rafiki wa karibu wa Mobutu Sese Seko.

Baba wa watoto watano amemuoa binti wa Mobutu na kusababisha kupewa jina “Mobutu Mdogo” kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na kiongozi huyo wa zamani wa DRC.

Novemba mwaka 1998 Bemba alibuni kundi la waasi MLC kwenye mkoa wake wa nyumbani wa Equateur.

Vikosi vyake baadaye vilihusika kwenye mzozo kati ya mwaka 2002 na 2003 kwenye nchi jirani ya DRC, vikipagana kwa ushirikiano na vikosi vilivyokuwa watiifu kwa aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ange-Felix Patasse, ambaye alikuwa akipingwa na aliyekuwa mkuu wake wa majeshi wakati huo Francois Bozize.

Agosti mwaka 1999, MLC ilisaini mkataba wa amani wa Lusaka ambao ulinuia kufikisha kikomo mapigano nchini DRC.

Aligeuza MLC kutoka kundi la waasi na kuwa chama cha kisiasa kufuatia kusainiwa makubaliano ya amani ya mwaka 2002.

Bemba alihudumu kama mmoja wa makamu wanne wa rais nchini DRC kwenye serikali ya umoja kati ya mwaka 2003 na 2006.

Kama mgombea mkuu wa chama chake aliwania urais mwaka 2006 lakini akashindwa na rais wa sasa Joseph Kabila, kwenye marudio.

Mwaka 2007, mapigano kati ya wapiganaji watiifu kwake na jeshi yalizuka mjini Kinshasa na kusababisha vifo vya takriban watu 100.

Bemba alikimbilia nchini Afrika Kusini akidai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini. Baadaye alikimbilia uhamishoni na familia yake.

Mwezi Mei mwaka 2008 alikamatwa na mahakama ya ICC mjini Brussels, Ubelgiji kujibu mashtaka ya uhalifu uliotendwa na vikosi vyake nchini Jamhuri ya Afrika ya kati.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents