Burudani

Mwanasoka Pekee anayenivutia ni Samatta – H. Polepole

Katibu wa itikadi, siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amemtaja mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta kama mwanasoka pekee anayemvutia nchini kwa sasa.

Polepole ameyazungumza hayo katika mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi, Tabata Relini, jijini Dar es Salaam, Polepole alisema juhudi za Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa (Taifa Stars) ndizo zinazofanya avutiwe naye.

“Napenda kuona vijana wetu wanapata mafanikio kwenye soka hivyo mchezaji wa soka ambaye ninampenda ni Mbwana Samatta.Huyo tu kwa upande wangu ndiye anatosha kwa ndani na nje ya nchi na hakuna mwingine anayenivutia zaidi yake,” alisema Polepole.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents