Tupo Nawe

Mwanaume ahukumiwa kwa sheria alizozitunga dhidi ya uzinzi Indonesia, kwa kuchapwa viboko 28- Video

Mwanaume ahukumiwa kwa sheria alizozitunga dhidi ya uzinzi Indonesia, kwa kuchapwa viboko 28- Video

Mwanaume mmoja nchini Indonesia aliyeweka sheria dhidi ya uzinzi ashikwa na kosa la uzinzi kwa kutembea na mke wa mtu. Mukhlis bin Muhammad kutoka baraza la Aceh Ulema amepigwa fimbo 28 kwa kosa la uzinzi. Mwanamke huyo ambaye alikuwa na mahusiano naye alichapwa fimbo 23.

Mukhlis anatokea katika mji pekee nchini Indonesia ambapo wanafuata sheria za kiislamu , zinazojulikana kama sharia.

Wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja pia wanaadhibiwa katika umati wa watu kwa kupigwa viboko.

“Hii ni sheria ya Mungu. Mtu yeyote anayekosea lazima aadhibiwe na sheria hizo,” Husaini Wahab, ni meya msaidizi wa eneo hilo la Aceh Besar aliiambia BBC.

Wapenzi hao walikamatwa na maafisa mwezi septemba, wakiwa katika gari ambalo lilikuwa limeegeshwa karibu na ufukwe wa kitalii.

Wapenzi hao walichapwa siku ya alhamisi, aliongeza bwana Husaini.

Mwanaume huyo aliyekamatwa ugoni ni kiongozi pia wa dini ya ya kiislamu.

Yeye ni kiongozi wa kwanza kupigwa katika kadamnasi kwa mujibu wa sharia iliyowekwa katika mji huo na kuanza kufanya kazi tangu mwaka 2005.

Afisa huyo ameshauri serikali ya mtaa na watunzi wa sheria ambao wanatekeleza sheria hiyo kufanya mabadiliko.

Aceh ilianzisha sheria ngumu za Kiislamu kwa zaidi ya muongo mmoja ili watu wapate haki zao.

Sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ilianzishwa mwaka 2014 na kuanza kufanya kazi mwaka uliofuata.

Kuwa na wapenzi wengi, kucheza kamali na matumizi ya pombe ni kinyume na sheria katika sharia ya kiislamu.

Mwaka 2017, wanaume wawili walipigwa fimbo 83 huko Aceh baada ya kukutwa wakifanya mapenzi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW