Habari

Mwanaume aliyepata ajali mbaya zaidi ya gari duniani, Aongea kwa mara ya kwanza

Hakuna linaloshindikana kwa Mungu, huu ni msemo ambao watu wengi huwa wanauchukulia poa lakini una maana kubwa sana kwa Ullas Kumar binadamu ambaye hakuna mtu kama alifikiri kuwa ataokoa maisha yake.

Ullas Kumar, 29 was impaled by a metal rod which went through his face when the car he was travelling in had a head on crash with a lorry
Ullas Kumar

Kumar (29) alipata ajali ya gari Machi 15, 2018 ambapo imeelezwa kuwa alikuwa kwenye Taxi kuelekea Uwanja wa ndege kumpokea kaka yake.

Kwa mujibu wa Gazeti la Hindu Times, Tax hiyo aliyokuwa anasafiria kabla ya kufika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kannur mjini Kannur, Tax hiyo iligongana na Lori uso kwa uso na ambapo dereva wa Taxi hiyo aliyejulikana kwa jina la Abdul Wahab alipoteza maisha papo hapo huku Kumar akitopbolewa fuvu la kichwa chake na chuma chenye umbo kama nondo.

Although the headrest is so close to Mr Kumar's eye doctors have said he was able to keep his eyesight 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa watu wote waliofika hapo waliogopa kumuokoa Kumar mpaka askari polisi walipotokea na kumpeleka hospitali.

Kumar alipelekwa katika Hospitali ya Aster MIMS mjini Kozhikode ambapo alifanikiwa kutolewa chuma hicho kwa upasuaji upasuaji wa masaa manne tu.

Following a four-hour operation doctors were able to remove the rod from Mr Kumar's head
Kumar baada ya matibabu

Kumar akinukuliwa na gazeti Hindu Times kwa mara ya kwanza amesema kuwa alikuwa kwenye Taxi kuelekea kumpokea kaka yake Uwanja wa ndege lakini ghafla alisikia mshindo mzito na kuanzia hapo hakuelewa kilichoendelea hadi alipozinduka Hospitalini.

Ninachokumbuka gari langu liligongana na lori lakini baada ya hapo nikaja kustuka Hospitali nikiwa na kichwa kizito huku nikitokwa damu sikufikiri kama ningekuwa hivi tena, kwani nilisikia kila sauti ya watu waliokuwa wamenibeba lakini sikuwa na nguvu ya kuongea wala kunyanyuka, najiona kama nimezaliwa upya,“amesema Kumar.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Rahul Menon amewapongeza madakatari wake kwa kufanya kazi nzuri kuokoa maisha ya Kumar.

Kutoa chuma kilichoingia kwenye fuvu la mgonjwa bila kuacha madhara yoyote kwa mgonjwa ni kazi nzito sana nawapongeza madaktari wangu wa kwenye kitengo cha upasuaji,“amesema Dkt. Menon.

Kumar amesema kuwa hakuamini kama angelipona au jicho lake kuona tena baada ya ajali hiyo lakini mpaka sasa ni mzima wa  afya na anaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail limeeleza kuwa ajali hiyo ni moja ya ajali mbaya zaidi ya gari kuwahi kutokea duniani.

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents