BizzareHabari

Mwanaume aliyevua viatu vinavyonuka kwenye basi ashikiliwa na polisi

Mwanaume mmoja jijini New Dehli nchini India amekamatwa na polisi kwa kosa la kuvua viatu vinavyotoa harufu mbaya kwenye basi la usafiri wa umma kwa kusababisha vurugu kwa abiria waliokuwa kwenye usafiri huo.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina Prakash Kumar (27) inaelezwa kuwa baada ya kuvua viatu hivyo abiria wenzake walianza kumshambulia kwa maneno wakimtaka ashuke kwenye gari lakini alikataa ndipo wakamuamuru dereva apeleke gari kwenye kituo cha polisi.

Gari hilo lililokuwa kwenye safari kutoka mjini Himachal Pradesh kuelekea jijini New Dehli lilimshusha kwenye kituo cha Polisi cha Bharwain nje kidogo ya Himachal ambako polisi walimzuia asiendelee na safari.

Tulimkamata Kumar baada ya kuletwa na Basi akivuruga amani kwenye Basi. “amesema Sanjeev Gandhi Kamanda wa polisi mjini Himachal Pradesh.

Gazeti la Hindustan Times la nchini India limeeleza kuwa bwana Kumar aliambiwa avitupe viatu vyake nje ya gari lakini alikataa kwa kudai kuwa vilikuwa havitoi harufu.

Polisi wamesema kuwa walimuachia masaa nane baadaye na kumsafirisha kwa basi lingine baada ya kumshikilia kituoni hapo ambapo alijitetea kwa kusema kuwa alishambulia bila kosa na abiria wenzake.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents