DStv Inogilee!

Mwanaume ukiwa na tabia hizi mbili; huwezi kuwa na Queen Darleen kwenye mahusiano

Msanii wa Bongo Flava, Queen Darleen ameeleza vitu viwili ambavyo mwanaume akimfanyia kwenye mahusiano hasiti kuachana naye mara moja.

Mwanadada huyo kutokea WCB akipiga stori na Funiko Base ya Radio Five ametaja vitu hivyo ni uongo na usaliti.

“Darleen kwenye mahusiano ni mtu ambaye hapendi uongo, hilo la kwanza, na akikaa na mtu anakaa na mtu lakini yule mtu akigundua kama amemsaliti hawezi kumsamehe,” amesema.

“Yaani umenisaliti na nina uhakika hata kama nakupenda vipi na tumeishi miaka mingapi mimi naachana na wewe kwa sababu imani yake Darleen atakapokusamehe basi utaendelea kuwa na mtu mwingine,” amesisitiza Darleen.

Queen Darleen ambaye ndiye msanii pekee wa kike katika label ya WCB, kwa kipindi kirefu hajaweka wazi mahusiano yake kitu kilichopelekea hivi karibuni kutaniwa na Lava Lava katika mtandao kwanini hamuweki wazi shemeji watu wamjue.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW