Habari

Mwandishi aliyeniandika vibaya akifika Machi mwakani akiwa hai naacha kuhubiri – Mzee wa Upako

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.
mzee-wa-upako3

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents