Habari

Mwandishi mkongwe auawa kwa kupigwa risasi India

By  | 

Mwandishi wa habari mkongwe nchini India, Gauri Lankesh mwenye miaka 55 amefariki dunia kwa kupigwa risasi majira ya jioni Jumanne hii.


Picha ya Gauri Lankesh enzi za uhai wake

Kifo cha Gauri ambaye alikuwa mhariri wa gazeti la kila wiki la Lankesh Patrike, kimetokea katika nyumba yake iliyopo mjini Bangalore.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi la nchini humo, limeripoti kuwa mwandishi huyo ameuawa kwa kupigwa risasi mara mbili kichwani na watu ambao walivamia nyumba yake wakiwa na pikipiki.

Hata hivyo hakuna mtu yoyote ambaye amekamatwa kwa tuhuma za tukio hilo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments