Habari

NIGERIA: Mwandishi wa BBC aliyerekodi Wahadhiri wakiomba rushwa ya ngono vyuoni, Yupo hatarini kuuawa

Mwandishi wa habari za kiuchunguzi wa Shirika la habari la BBC, Kiki Mordi ambaye  alifanyakazi ya kupeleleza vitendo vya rushwa ya ngono kati ya Wahadhiri wa kiume na wanafunzi wa kike katika vyuo vikuu viwili vya Ghana na cha Lagos nchini Nigeria, Ametangaza kupokea vitisho vya kuuawa.

Image result for Kiki Mordi

 

Kiki ambaye yeye mwenyewe amekiri kuwahi kuombwa rushwa ya ngono akiwa chuoni, Amesema kuwa amepokea vitisho hivyo mapema baada ya BBC kuachia Documentary yake inayowaonesha Wahadhiri wa vyuo hivyo wakimuomba rushwa ya ngono, Jambo lililopelekea Mhadhiri mmoja wa chuo cha Lagos, Dkt. Bonniface Igbineghu kusimamishwa kazi huku wengine wakipelelezwa.

Akihojiwa na mtandao wa Sahara Reporters, Kiki amesema “Napokea vitisho vingi kupitia meseji, Mitandao ya kijamii, Napigiwa simu naambiwa siku zangu zinahesabika lakini siogopi kwa vile nilichokifanya ni historia kamili ya maisha yangu. Mimi niliombwa rushwa ya ngono kwa ahadi ya kupewa alama nzuri darasani! Nikakataa na baada ya hapo sikufanikiwa kufaulu hadi nikaacha Chuo. Hilo mimi siogopi nitakufa kwa ajili ya ukweli sina hofu na najua BBC wananilinda kwa hilo.“.

Hata hivyo, Bado naendelea na mafunzo zaidi. Najua kazi hii niliyofanya imebadilisha jamii kimtazamo, Hilo ndio jambo ninalojivunia hata nikifa leo. Najua moja ya Mhadhiri wa chuo cha Lagos kashasimamishwa kazi na Mamlaka husika, Nataka isiishie hapo ikibidi ashtakiwe, Mapambano kwa upande wangu bado yanaendelea,“amesema Kiki.

Wiki iliyopita Kiki alijizolea umaarufu barani Afrika, Hususani Afrika Magharibi na Kaskazini kufuatia Documentary yake ya kiuchunguzi wa rushwa ya ngono vyuoni, Kurushwa na kituo cha BBC.

Kiki Mordi ambaye ni raia wa Nigeria, Anafanya kazi na BBC Africa Eye, Amesema kuwa alikata tamaa kutoka kwa Documentary hiyo kwani imekaa muda mrefu wa zaidi ya miezi 11.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents