Habari

Mwandishi wa habari aliyejibizana na Donald Trump Ikulu, arejeshewa kibali chake kilichofutwa

Mwandishi wa habari aliyejibizana na Donald Trump Ikulu, arejeshewa kibali chake kilichofutwa

Ikulu ya Marekani imerejesha vibali vya mwandishi wa habari wa shirika la CNN chini ya wiki mbili baada ya kufuta vibali hivyo kufuatia majibizano na Rais Donald Trump wakati wa mkutano na waandihi wa habari. Hii ni siku kadhaa baada ya jaji kuamrisha uongozi wa Trump kumrejeshea mwandishi huyo kibali hicho.

Kwa mujibu wa BBC, Ikitangaza uamuzi wake, Ikulu ya Marekani pia ilitangaza sheria ambazo zitaongoza mikutano ya baadaye huko White House. Hii ni pamoja na swali moja kwa kila mwandishi wa habari. Maswali mengine zaidi yataruhusiwa kwa ruhusa ya rais au afisa ndani ya White House, kwa mujibu wa barua iliyotumwa. Barua hiyo pia ilionya kuwa hatua zuidi zitachukuliwa dhidi ya Acosta ikiwa hatafuata sheria hizo mpya. Akizungumzia uamuzi huo wa siku ya Jumatatu wa kurejeshewa vibali vyake, Acosta alisema anataka kurudi tena White House.

Mzozo ulianza kwa njia gani?

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, mfanyakazi wa lkulu alijaribu kuchukua kipasa sauti kutoka kwa Bw Acosta wakati alijaibu kumuuliza Bw Trump maswali zaidi. Bw Trump alimuita Acosta mtu mbaya na mwandishi huyo akazuiwa kuingia Ikulu siku moja baadaye. CNN ilipeleka kesi mahakamani kutaka vibali vya Acosta kurejeswa na ikaungwa mkono na vyombo vingine vya habari kikiwemo cha Fox News.

Wakati wa kutolewa uamuzi siku ya Ijumaa jajii mjini Washington alisema uongozi hhaukuwa na sababu za kutosha za kufuta vibali hivyo.

Ikulu ilisema nini baada ya mzozo?

Bi Sanders katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa twitter alisema Ikulu haiwezi kuvumilia kamwe mwandishi anayeweka mikoni yake kwa mwanamke mchanga anayejaribu kufanya kazi yake. “Ukweli kuwa CNN inajivunia kile mfanyakazi wao alifanya sio tu cha kughadhabisha, ni mfano wa kukosa heshima kwa kila mtu, akiwemo mwanamke ambaye anafanya kazi katika uongozi huu,” alisema.

Trump anafaa kuwa na hofu uchaguzi Marekani?. Kutokana na hili , Ikulu inafuta kibali cha kuingia cha mwandishi wa habari aliyehusika hadi wakati usiojulikana. Bw Acosta kwa njia ya Twitter alisema alizuiwa na kikosi cha kumlinda rais kuingia uwanja wa Ikulu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents