Habari

Mwandishi wa habari Mkenya wa kituo cha Al Jazeera aachiwa baada ya kuwekwa kizuizini huko Niger!

Mwandishi wa habari kutoka Kenya Yvonne Ndege na crew yake inayojumuisha mpiga picha, producer na dereva walikamatwa na kuwekwa kizuizini huko Zinder, kusini mwa nchi ya Niger.

Yvonne

Mtandao wa Ghafla wa Kenya umeripoti kuwa Yvonne na crew yake wameachiwa huru jana Jumatatu (June 17) baada ya kutiwa kizuizini toka Jumamosi (June 15).

Baada ya mwandishi huyo na team yake kuwekwa kizuizini Jumamosi walihojiwa na kuamrishwa kukabidhi picha zote za video ya story ya wakimbizi waliyokuwa wanakusanya nchini humo.

Kituo cha Al Jazeera kimewashukuru wote waliosaidia wafanyakazi wao kurudi salama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents