Tupo Nawe

MWANZA: Mwalimu atupwa jela mwaka mmoja kisa rushwa ya ngono kwa mzazi wa mwanafunzi wake

Mahakama Wilayani Ilemela jijini Mwanza, imemhukumu mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Jabal Hirah, Mwatanda Omari (37) kifungo cha miezi 12 jela kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono.

Image result for rushwa ya ngono

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatano Mei 15, 2019 na mkuu wa Takukuru mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga imedai kuwa hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi wa manispaa ya halmashauri ya wilaya ya Ilemela, Abesizya Kalegeya baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Imeelezwa kuwa Mwalimu mkuu huyo alitaka apewe ngono ndipo aweze kujaza fomu ya uhamisho kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

Kwa mujibu wa taratibu za kiutendaji Mwalimu Mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kujaza fomu ya uhamisho kwenye shule husika.

Kwa upande wa Jamhuri ukiongozwa na mwanasheria wa Takukuru, Placidia Rugalema ulidai kuwa mwalimu huyo alitenda kosa hilo Machi 9, 2017 kwa kumuomba ngono mzazi wa mwanafunzi aliyekuwa anaomba uhamisho wa mtoto wake kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.

Akijitetea mahakamani, Mshtakiwa kwa upande wake aliiomba mahakama imsamehe kwa kuwa hakutenda kosa hilo kwa kukusudia, hata hivyo mahakama ilimpa adhabu ya kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya TSh Milioni 2.5  ambapo alishindwa kulipa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW