Burudani

Mwanzilishi wa Death Row Records, Suge Knight ashtakiwa kwa mauaji

Mwanzilishi wa Death Row Records, Suge Knight ameshtakiwa kwa kuhusika na mauaji na pia kujaribu kuua baada ya kuwagonga kwa gari watu wawili kufuatia majibizano huko Compton wiki iliyopita.

056679_knight__

Anaweza kufungwa kifungo cha maisha kama akipatikana na hatia.

Mashtaka rasmi yamekuja baada ya dhamana yake ya dola milioni 2.2 kukataliwa. Knight, 49, anashtakiwa kwa kuwagonga na gari is Terry Carter na Cle “Bone” Sloan. Carter alifariki.

Knight anatarajiwa kupanda kizambani kwa mara ya kwanza Compton Jumanne hii.

Knight alianzisha Death Row Records akiwa na Dr. Dre mwaka 1991 na kuanzisha label ya kwanza ya hip hop iliyotawala muziki huo enzi hizo.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents