Habari

Mwanzilishi wa Jamii Forums apewa dhamana

Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo Jumatatu hii, ameachiwa huru na Hakimu Godfrey Mwambapa wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.

Wadhamini hao kila mmoja amesaini dhamana ya maneno ya shilingi milioni 5. Max ambaye ni mwanzilishi wa mtandao huo ameshikiliwa na polisi tangu Jumanne wiki iliyopita akishtakiwa kwa makosa matatu.

Miongoni mwa makosa hayo ni kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa na kuzuia uchunguzi wa polisi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa Kimtandao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents