Habari

Mwanzilishi wa Kampuni ya Alibaba Jack Ma amtaja atakayechukua nafasi yake baada ya kustaafu

Mwanzilishi wa Kampuni ya Alibaba Jack Ma amtaja atakayechukua nafasi yake baada ya kustaafu

Jack Ma, ni mwanzilishi wa kampuni kubwa ya Kichina ya Alibaba Group, ametangaza rasmi kustaafu katika cheo chake kama C.E.O. Akiwa na umri wa miaka 54 amesema kwamba Daniel Zhang atachukua utawala katika nafasi yake ya mwenyekiti wa kampuni hiyo, ingawa Ma atabaki kwenye bodi ya wakurugenzi wa Alibaba mpaka 2020.

Katika barua ya wazi kwa wafanyakazi wake, wanahisa na wateja wake, Ma alisisitiza kiasi na muda alioutumia katika kuchagua mrithi wake, akigusa nafasi yake ya awali kama mwalimu katika mchakato. “Walimu daima wanataka wanafunzi wao kufanya makubwa kuwazidi wao,”

aliongeza Ma. “Kitu kinachonihusisha mimi na kampuni kufanya ni kuruhusu watu wadogo wafanye kazi, wenye vipaji zaidi kuchukua nafasi katika majukumu ya uongozi ili waweze kurithi kazi yetu.” Alibainisha kuwa kampuni hiyo ilifurahia mabadiliko mazuri mwaka 2013, wakati Zhang alichukua Jukumu la Ma na kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Akitoa mfano wa mfumo wa ushirikiano wa Alibaba na “usawa kati ya mfumo, watu na utamaduni” kama mali ya binadamu yenye nguvu sana. Baada ya Ma kustaafu kampuni, ina mpango wa kuizingatia Jack Ma Foundation, kushirikiana na Bill Gates, kwa kufanya kazi kusaidia mfumo wa elimu ya vijijini nchini China.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents