Burudani

Mwarabu Fighter “Nilianza kupata hela baada ya kuachana na Diamond, Wananiimba kwenye nyimbo zao ukweli wanaujua” – Video

Mwarabu Fighter "Nilianza kupata hela baada ya kuachana na Diamond, Wananiimba kwenye nyimbo zao ukweli wanaujua" - Video

Aliyewahikuwa Bodygurd wa Diamond Platnumz Mwarabu Fighter amefunguka mengi kuhusu maisha yake ya sasa na yale maisha aliyoishi wakati akifanya akzi na Diamond Platnumz.

Akipiga stori na Bongo5 Mwarabu Fighter amesema kuwa:- ” Nilipoancha kazi nilihangaika sana maana sikuwa na hata sent mia, mke wangu aliuza genge mtaani ili tupate chochote, Vijana wengi wajifunze kupitia kwangu. mimi niliishi ili kulinda Brand ya Diamond haliyakuwa mfukoni sina kitu, niliishi ili niendane na Brand ya msanii mkubwa lakini katika nafsi yangu nilimia sana, Wakati huo sikuwa na gari wala pikipiki wala chombo chochote cha usafiri lakini nilikuwa napanda magari ya kulipi” Mwarabu aliongeza “Mshahara wangu haukutosha hata kwa wiki mbili lakini sikuwa na namna”

Mbali na hilo mwarabu amezungumzia kuhusu kuzungumziwa na kuimbwa kwenye nyimbo na wasanii wa WCB hasa Diamond Platnumz kwenye wimbo wake wa Inama na Harmonize_tz kwenye wimbo wake alioshirikiana na Q Chillah My Boo kuhusiana na mpenzi wa Harmonize Sarah, kuhusu ilivyokuwa ikidaiwa walikuwa wakitoka kimapenzi. Mwarabu amefunguka haya.
“Ukweli wanao wao Diamondplatnumz anaujua ukweli lakini pia Harmonize anaujua ukweli, wao wanatumia nyimbo zao kufikisha ujumbe lakini hawataki kuongea ukweli, Mi nafurahi wanavyoniongelea kwani bado wanakumbuka makubwa niliyowafanyia”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents