Burudani

Mwasiti adai nafasi yake kwenye muziki ipo pale pale

Mwasiti anaamini kuwa nafasi yake kwenye muziki ipo pale pale tofauti na baadhi ya watu wanaodhani kuwa amepotezwa na wasanii wapya wa kike walioibuka hivi karibuni.

3d3d1d34d1ff11e399ae0002c9dca842_8

“Kila mmoja ana ladha yake, na kila mmoja ana nafasi yake, mimi nipo na nitaendelea kuwepo na hakuna anayenitisha.” Mwasiti aliiambia tovuti ya Times FM.

Pamoja na hivyo, Mwasiti amewapongeza wasanii wapya wa kike walioibuka na kufanya vizuri huku akiwatahadharisha kuwa makini kwenye kazi zao.

Pia amedai kuwa utaratibu wake wa tangu 2009 enzi za wimbo wake wa ‘Nalivua Pendo’ wa kuachia single moja moja kila mwaka utaendelea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents