Habari

Mwasiti asema muziki hauflow kama maji, unahitaji juhudi

Hitmaker wa Mapito, Mwasiti Almas, amewakumbusha vijana wanaotaka kuchomoza kwenye muziki kuwa kamwe muziki hauflow kama maji bali unahitaji juhudi.

20

Akiongea na Kali za Bomba ya Bomba FM leo, Mwasiti amesema ili ufanikiwe ni lazima ujitume na ujue unachokitaka.

“Kuliko kuliko vyote, unataka nini ndani ya muziki,” amesema.

“Ni vizuri ukajua kabisa kwamba hii ni biashara. Na biashara products zinaweza kuwa zinafanana kwa uso lakini zikawa na ladha tofauti. As long as unafanya kazi na unajua unataka nini hata competition yenyewe itakuwa inakupa tu challenge sio kwamba inakutisha.”

Katika hatua nyingine, Mwasiti amesema anatarajia kuachia wimbo mpya mwisho wa mwezi huu. “Nimejaribu kuimba katika miondoko tofauti kidogo, hata ukisikiliza utaona kuna utofauti mkubwa sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents