Burudani

Mwasiti, Linah na Vanessa Mdee waongelea jinsi wimbo wa Fistula ulivyowaunganisha wasanii wa kike

Video ya wimbo wa wasanii wote wa kike wa Tanzania ‘Kidole Kimoja’ ulioimbwa kwaajili ya kampeni dhidi ya ugonjwa Fistula imetoka. Ni video yenye muonekano mzuri na inayovutia, iliyofanywa na kampuni ya Redline Productions.

linan na vee

Video hiyo imefanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani. Katika wimbo huo ulioandikwa na kutayarishwa na Nash Designer, zaidi ya wasanii wa kike 15 wameshiriki.

“Mimi binafsi kwa mara ya kwanza niliweza kukutana na wanamuziki wengi wa kike kwa pamoja, ni nadra sana kitu kama hicho kutokea halafu ni kizazi chetu. Kwahiyo it was good kiukweli, tulijuana ipasavy, watu walikuwa wanaogopana lakini wakajuana vizuri, ushirikiano ulikuwa mzuri toka kwa mwanamuziki mmoja kwenda kwa mwingine, “ amesema Mwasiti kuelezea jinsi mradio huo ulivyowaunganisha.

http://www.youtube.com/watch?v=jUaDqdwfhoU&feature=player_embedded

Naye Vanessa Mdee amesema, “unajua mara kwa mara we don’t get to hang out hivyo na wasanii kwa hiyo mimi niliienjoy na kupata nafasi ya kucheal na wasanii wa kike wengi hivyo na kuexchange ideas. Tulidrive mpaka Mkuranga tulitumia masaa matatu, kwahiyo tunapiga story, wenye kuimba tunaimba wote rendition za nyimbo tofauti, it was really fun.”

Kwa upande wake Linah, safari ya kwenda kufanya video hiyo iliweza kumuongezea marafiki atakaoshirikiana nayo siku za usoni.

“Tumekutana wasichana wote ambao tunafanya muziki wa Bongo Flava kwahiyo tumeweza kujuana, kusomana, nimeweza kumfahamu flani ameweza kunifahamu mimi. Kiukweli siku hiyo nimeongea sana na my dada Vanessa, tumeongea mengi, ushauri kutiana moyo vitu kama hivyo. Mimi na Vanessa tunaweza tukafanya kitu.”

Wasikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents