Michezo

Mwenyekiti mpya Yanga, Dkt Mshindo Msolla ataja mambo mawili muhimu atakayoanza nayo/amtaja Mwinyi Zahera na mechi zilizobakia (+video)

Klabu ya Yanga hapo jana imepata uongozi mpya kuanzia ngazi ya Mwenyekiti, makamu Mwenyekiti na wajumbe baada ya kufanyika uchaguzi mkuu katika kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar Es Salaam. Mara baada ya kushinda katika nafasi ya Mwenyekiti, Dkt Mshindo Msolla ameahidi kumpatia fungu la kutosha kocha mkuu wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera ili kuhakikisha anakuwa na kikosi imara na chenye kuleta ushindani.

”Yakwanza muhimu ni kuhakikisha hizi mechi za mwisho zinachezwa, kwa timu zote mbili Yanga ya wakubwa na ile Yanga Princes,” amesema Dkt Mshindo Msolla

”Lapili ambalo ni la haraka ni kutafuta pesa kwaajili ya Zahera aweze kusajili aweze kusajili wachezaji anao wahitaji ili aweze kujenga kikosi bora.”

Klabu ya Yanga imemchagua Dkt. Mshindo Msolla kuwa mwenyekiti wake huku Fredrick Mwakalebela akishinda katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Dkt. Msola amepata kura 1,276 akimshinda mpinzani wake Dkt. Jonas Tiboroha aliyepata kura 60.Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwakalebela amepata kuara 1,206 akiwashinda Janneth Mbene aliyepata kura 61, Titus Osoro aliyepata kura 17, Yono Kevela aliyepata kura 31 na Chota Chota aliyepata kura 12.

https://www.instagram.com/p/BxF9zgmgIcO/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents